Bismillah Rahman Raheem..
Karibu tena Akhy/ukhty yangu katika makala hii yako pendwa tukiangazia mambo mbalimbali hukusu Uislam wetu..
Karibu..
Allah anasema katika Qur’an tukufu..
{ يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا أَصَابَكَ ۖ إِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ }
[Surah Luqmân: 17]
Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo yanayohitaji azma..
Point ya kunote hapa ni hiki kipande..
إِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ...
Hayo ni katika mambo yanayohitaji azma.. yanayohitaji kuyapania, kuyawekea mikakati maalum..
Mzee Luqman Al Hakim, Allah anamnukuu akituambia sisi vijana wake..
"Bila determination (azma) hutofanya la kheri.."
Mfano..
Kushika Swala..
Bila kuwa na azma na mikakati maalum ya kusimamisha swala 5 kwa siku, hutoboi..
Licha ya kuwa Allah amekuafikisha, Ila na wewe nafsini mwako na kwenye mazingira yako unayakwepa mengi ili uweze kusimamisha swala 5.
Umeazimia, umepania..
Na katika hilo, huenda unaacha shughuli zako za msingi. Maongezi yako na watu wenye thaman kwako. kwakuwa umeazimia swala 5 kwa siku..
Kuamrisha mema, kukataza maovu..
Mfano mwingine katika kuamrisha mema na kukataza maovu..
Hapa vipo vingi ndani yake..
Kwanza, huwezi kuamrisha mema na kukataza maovu kama wewe haujajikataza maovu na hujajiamrisha mema..
Na katika kujiamrisha mema na kujikataza maovu panahitaji AZMA..
Uazimie kufanya mema hata kama hayakufurahishi na usifanye maovu hatakama unayapenda..
Pia Uitafute elimu, ili uweze kuamrisha mema na kukataza maovu kwa elimu hio..
Lakini bila kuazimia kutulia na kuisoma. Ni ngumu kupata elimu..
Pia huenda kwa kuamrisha mema na kukataza maovu. Ukawakosa marafik zako wa karibu unaowapenda, Ukadharaulika, Ukateswa, na ukateseka kwa ajili ya da'awah..
Lakin kwakuwa uliweka Azma. Basi hujali hata!
Na pia hata kama ikitokea umefanya
maasia mengi vipi, dhambi na uovu..
Ila kwakuwa uliweka Azma ya kuswali swala 5 kwa siku. Uliazimia kusoma Qur'an kwa siku walau karatas moja..
Basi huruhusu dhambi hio au ovu hilo liwe sababu ya kuondoa azma yako..
Subra..
Pia unaweza fikwa na Hali flan katika maisha ambayo hali hio inahitaji Subra..
Basi hio Subra pia yahitaji maazimio..
Ikiwa ni ugonjwa..
Wapo watakao kwambia "Kuna mganga kutoka ufipa.."
Kama hujaazimia Subra, utaenda tu..
Ikiwa ni umaskini, maokoto hayaokoteki..
Wapo watakao kwambia..
"Mkeka wa muhindi, odds nyingi.."(Betting)
"Riba nafuu.."(Interest)
"Turushe kindege.."(aviator)
"Tutapeli.."(dhulma)
Ikiwa hujaazimia kusubiri, utafanya yasiyofaa ili ukidhi haja ya umasikin wako kwa haram na ikawa ni khasara kwako..
Kwahivo jitaahid kushikamana na azma..
Maana inafika Hali umechoka. Ila bila azma, bila kupania kufanya hio amali ya kheri. Utashindwa..
Bila azma, mikakati maalum, na kupania, kung'ang'ania. Kuwa king'ang'anizi
Bila kuzikataa destructions na wasiwasi za shaytwan..
Hio page 1 ya Qur'an uliopanga uifute kila siku, hutoifuta. Au ule mpango wako wa Kuhifadhi Qur'an hutotimia kama hujaazimia kuacha kusikiliza miziki na kujizatiti..
Zile rakaa 12 za baadia na Kablia hutazidumisha..
Lile darsa ulilopanga kwenda kila siku hutoenda..
Kile kitabu cha Fiqh ulichoanza kukisoma, hutakimaliza..
Hata Ile Dhikr ya baada ya swala ya Faradhi..
Kusema Subhanallah, Alhamdulillah, Allahu Akbar mara 33..
Wallah ni ngumu, bila azma..
Uwe determined, na usifuate destruction, usifuate vyenye kukutoa katika njia yako, katika azma yako. Ambavo vingi ni michezo ya shaitwan na wasiwasi wake..
Simu, Social media, games, thamthilia, movies, umbea na marafik, miziki, mpira, usingizi, uvivu na mengine ambayo hukupotezea wakati..
Allah anatuambia..
{ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ }
[Surah Al-An âm: 153]
Wala msifuate destructions, zikakutengeni na njia yake Allah..
Hivo ukishaazimia kukaa katika njia ya Allah..
Yani ushasema hii njia ya Allah nalala nayo, ama nusra, ama Jannah..
Basi destructions zitakuja, na zipo ila inabidi uzikatae, na kumbuka umeazimia..
Kwahivo..
Ibada hizi, na yote ya kheri..
Ni azma, ari, kupania, kung'ang'ania..🏃🏽♂️
Consistency, pumzi nyingi, pushup za kutosha, maji mengi..😄
We unadhani kwanini ikaitwa Jihadunnafs??😄
Ni mimi Akhy yako Mubaarak..
Usinisahau kwenye dua zako..
Nilikuwepo, Assalam alaykum..😄🏃🏽♂️
Kama una maoni, ushauri au unataka kunisalimia Muislam mwenzio. Nichek Whatsapp..