Hautashindwa Kuamka Tahajjud Tena...!
Ukiyajua matano (3) haya kuamka kusali Tahajjud kwako itakuwa ni kugusa Tu, Biidhnillah!. Jambo la 2 katika haya 3 litakushangaza.. Shuka nami๐๐ผ๐
Bismillah Ar Rahmani Rahiim.
Assalam alaykum warahmatullah wabarakatuh..
Karibu tena katika makala hii ya Ahadun Ahad, mahali ambapo ni sahihi kwa ajili ya Imaan yako..
Naam, Huenda na wewe ni miongoni mwa watu wanao struggle kuamka kusali Tahajjud..
Umeset alarm, lakini wapi..๐คฆ๐ฝโโ๏ธ
Umejitahid ulale mapema, wapi wee..๐คฆ๐ฝโโ๏ธ
Ukaomba hadi mtu akuamshe lakini aise kwan uliamka basi..๐
Sasa tunapoongelea swala la kuweza kuamka usiku na kuswali Tahajjud ndio lazima ujiandae, yaani..
Ulale mapema ukiwa twahara(wudhu), usome adhkaar za kulala, na uweke Nia ya kuamka kuswali (At least ulipwe kwa Nia).
Lakini sasa, maandalizi yoote yanachukua 30% - 40% ya kukuwezesha kuamka usiku..
Sasa, hio 60% - 70% imechukuliwa na nini?.
Leo In Shaa Allah, nitakueleza biidhnillah hilo..
Basi Shuka nami..
๐๐ผ๐๐ผ
Na naamin, ukishalifahamu hilo na ukalifanyia kazi, In Shaa Allah, kuamka kwako usiku itakuwa ni kugusa Tu.. Paap!, Maa Shaa Allah..๐
Asilimia 70% ya kuweza kuamka kwako usiku, kumebebwa juu ya mambo matatu (3)
Naam, mambo yenyewe ni..
Uzito wa Moyo..
Ndio, Ni uzito wa Moyo..
Moyo ndo uliobeba mwili, Kwahio mgumu kuamka si wewe, Bali ni moyo wako.
Baadhi ya watu husema moyo ni kama sponji, hunyonya vitu vile ambavyo tunavifanya katika maisha yetu na kutunza. Hivo kama sponji ukilinywesha maji mengi ndo linavozidi kuwa zito, basi na moyo wako vivo hivo..
Na moyo huwa mzito kutokana na kubeba vitu kama ; -
Unafiki, chuki, kumsengenya mtu nafsin mwako peke yako, kumsema mtu kwa ubaya nafsini mwako, vinyongo, visasi, hasira n.k..
Hivi ndo vitu ambavyo ukivinywesha na kuuzoesha moyo wako kuvibeba basi, aisee kuamka kwako usiku itakuwa ngumu..
Na kuthibitisha hili, hebu tufikirie kuhusu Aya hii ya Allah, akieleza sifa za wanafiki.
Tukumbuke kuwa unafiki, unaendana sawasawa na maradhi mengine ya moyo kama hasadi, chuki, na kupenda kusengenya ima iwe ni kwa nafsi yako au na mtu..
Allah subhanahu wa taala anasema..
[ ููุฅูุฐูุง ููุงู ููุง ุฅูููู ุงูุตููููุงุฉู ููุงู ููุง ููุณูุงููููฐ ููุฑูุงุกูููู ุงููููุงุณู ููููุง ููุฐูููุฑูููู ุงูููููู ุฅูููููู
Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu ili waonekane na watu na wanamdhukuru Allah kidogo tu.
[An nissa : 142]
Allah anatueleza katika Aya hii kuwa wanafik huwa ni wavivu wa kuswali kutokana na nifaq katik mioyo yao.
Na huswali kwasababu ya kuwaonesha watu, na swala hizi huwa ni swala za jamaa, swala ambazo watu wapo na huzihudhuria..
Sasa kama ana uvivu juu ya swala hizi za faradhi, vipi hali yake katika swala ya kuamka usiku?, Itakuwa ni kazi mno kwake, uvivu mara mbili ya huo.
Na isitoshe, amuoneshe Nani kuwa anaswali usiku?, hivo hatoweza kuamka ataendelea kulala..
Na Aya hii, au uvivu wa kwenye Aya hio unaeleza Hali hio ipo kwa kila ambae moyo wake una maradhi, basi atakuwa na Uzito na uvivu..
Na pia tukiangalia katika Hadeeth ya Mtume Salallahu alayhi wa salam..
ููุงู ุงููุจู ๏ทบ: ุฃุซูู ุงูุตูุงุฉ ุนูู ุงูู ูุงูููู ุตูุงุฉ ุงูุนุดุงุก ูุตูุงุฉ ุงููุฌุฑ
"Swala nzito, yenye kuwatia uvivu wanafik ni swala ya Ishaa na alfajir.."
[Bukhari & Muslim]
Hii pia ni dalili ambayo yaonesha uzito wa mtu mwenye maradhi nyoyoni mwake anashindwa kuamka usiku kutokana na Uzito wa moyo wake kwasababu umebeba unafik n.k..
Anashindwa kuamka kuswali fajr kwa jamaa, unadhan ataweza kuamka usiku??
Sijui umeanza kunipata pata Akhy/ukhty..
Allah atutibu maradhi ya Moyo na aifanye iwe miepesi, amiin..
Labda nikupe hichi kisa hiki kizuri hapa chini, huenda kikakuongezea uelewa..
Imepokewa kutoka kwa Abu Talib al-Makki:
Sufyan al-Thawri,Rahimahullah, alisema:
"Nilinyimwa kuamka swala ya usiku kwa miezi mitano kwa sababu ya dhambi niliyofanya."
Akaulizwa, "dhambi gani?"
Sufyan akasema, "Nilimwona mtu analiana nikajiambia(moyoni): Huyu nae anajionyesha.."๐
Qut al-Qulรผb : 1/75]
Nimeeka emoji ili ulete ule uhalisia๐..
Sasa tunaona alichokifanya Sufyan mpaka akashindwa kuamka kuswali usiku kwa miez mitano. Ni alimsengenya mtu na kumdhania vibaya katika nafsi yake..
Hii Hali tunayo sana sisi, siku hizi. Tunasengenya na kusema watu vibaya na kudhani vibaya watu kupitia nafsi zetu..
Hivyo ikiwa tunatamani tuwe watu wa usiku, Waja wa Allah wenye kuamka usiku, basi tukamue mioyo yetu na tuisafishe kutokana na chuki, hasadi, visasi, n.k
Nadhani pia hii ndo Sababu Rasulullah, Salallahu alayh wa salam akakufundisha kutokulala na vinyongo na kusamehe kabla hujalala..
Ili kuuweka moyo wako katika wepesi wa kuweza kuamka usiku. Na kuuondosha ugumu wa Moyo..
Usikilize moyo wako nini unasema au unahisi kuhusu mtu fulan au watu Fulani..
Ikiwa moyo Una hisia mbaya na dhana mbaya kwa watu basi ukataze..
Haya tuendelee..
Jambo la Pili ni
Chunga matendo ya mchana..
Hilo ni kumaanisha kuwa..
chunga matendo yako ya mchana kwa kujitaahidi kuyatengeneza yawe ni matendo mema kwa wingi..
Fanya matendo mema, ongea kauli njema, samehe aliokukosea, omba radhi kwa uliemkosea, nasiha, dhikr ya Allah..
Kuwa na Nia nzuri katika unayoyafanya, kujali watu, kusaidia watu, kujijali wewe n.k..
Hii ni kwasababu..
matendo hayo mema na mazuri ya mchana ndio kama kichocheo cha wewe kupata nguvu ya kuamka usiku..
Ukiufanya mchana wako kwa fujo na kutokufanya matendo mazuri..
Huenda ukalala na vinyongo na visasi, ukawa ushautia moyo uzito katika kuamka usiku..
Kwahivo fanya matendo mema mchana, upate cheche na nguvu ya kuweza kukuamsha usiku
Na utakaposwali usiku, Faida yake ni utapata cheche na nguvu ya kufanya matendo mema mchana..
Na utakapo fanya matendo mema mchana, utapata cheche na nguvu ya kuamka usiku.
Kisha mzunguko unaanza moja..๐
Huo inaitwa Mzunguko Mzuri Wa Tahajjud..๐
Naam na jambo la 3, na la mwisho ni
Kutokula sana usiku..
Hii ni kwasababu kula sana usiku, huufanya mwili uwe mzito. Kulewa na utashindwa kuamka usiku..
Naam, kwahio ukivizingatia vitatu hivo, baasi..
Kuamka wewe usiku, Biidhnillah, ni kugusa Tu. Na hapo ndo natia tamati juu ya makala hii ya Leo.
Kama umepata Faida juu ya Darsa hii, usisahau kunipa mrejesho kwa namba yangu ya Whatsapp. Bonyeza hapo chini
Ni Mimi Al Akh. Mubaarak,
Ahadun Ahad Studio,
Onja Ladha Ya Imaan.
Assalam alaykum..