Hijja Ndani Ya Moyo Wako Na Maisha Yako Ya Kila Siku..
Nimeandika Yale Ambayo Utajifunza Kupitia Hajj Na Yakufae Katika Maisha Yako Ya Kila Siku..
Nilikuwa nasikiliza darsa ya tafsir ya Qur’an kutoka kwa Ustadhat Taiymiyyah Zubair..
Namuelewa sana huyu dada, yani namna anavyoichambua Qur’an, Maa Shaa Allah😋
Anaizungumzia Qur’an kwa uzito wa Ilmu, upendo, na uchambuzi wa kina wa Lugha ya Qur'an..🙌🏽
Kiasi ya kwamba unajikuta upo ndani ya aya unazozisikia kutoka kwake. Allah ambaarik!🙂
Sasa juzi kati, nikisikiliza tafsir ya Suratul Hajj, Aya ya 25 hadi 28 — aya zinazogusia Hijja. Aliichambua kwa kina, na kugusa moyo wangu na kunifanya nifikirie upya namna ninavyoitazama ibada hii tukufu..
Na hapo ndipo iliponijia wazo la kuandika kuhusu “Hijja ndani ya mioyo na maisha yetu ya kila siku”
Katika hili nitaandika mambo 7 ya kujifunza katika Hijja kwa ujumla. Allah ajaalie niyafikishe kwako kwa ukamilifu wake..
Jambo la 7 litakushangaza, hivo baki nami hadi mwisho..
Matokeo Ya Ikhlaas.
Miongoni mwa tunayojifunza ni matokeo ya kufanya jambo kwa NIA ya kwa ajili ya Allah, na IKHLAS kuwa Allah ndo anaeyafanya mambo yawe, si nguvu zetu wala akili zetu..
Nabii Ibrahim alayh salaam, alipoambiwa awaite watu, hakuwa na sauti hio ya kuweza kuwafikia watu wote Duniani. Lakin aliita akiwa na Ikhlas kuwa Allah ndie anaefanikisha jambo, wala si sauti yake..
Na kutokana na ikhlas yake, Allah akatia barakah kupitia sauti yake, watu hadi Leo wanaitika wito wake, wito ambao Allah ametuita kupitia yeye..
Na hio ni Barakah itokayo kwa kufanya jambo kwa ikhlas, na Nia kwa ajili ya Allah..
Hujui Ni Neema Gani Allah amekuandalia Juu Ya Mazito Unayopitia..
Kama alivosema Allah, “hakika penye uzito kuna wepesi..” Ijapo wengi wetu hatuwazi kabisa huo wepesi unaokuja baada ya uzito, Ila tunanung’unika na kujihisi hatuna bahat linapotupata zito..
Lakin ni vema uamin na uutulize moyo wako kuwa inabidi upite katika hali fulan, nzito, ngumu, ya kuchosha ili uweze kupata kile cha kheri alichokuandalia Allah..
MwanaHajar, mama yake Ismail alipoachwa peke ake jangwani, na Ismail ni mdogo analalamika kiu. Ilibidi mwanaHajar a-hustle sasa, wapi atapata maji, mara saffa, kisha Marwa, round kadhaa, kisha ndo Allah kwa uweza wake akayatoa maji ya Zamzam..
Maji ambayo ikawa miliki yake mwanaHajar. Sidhan kama Allah aliishindwa kuitoa chemchem ya Zamzam kabla mwanaHajar hajaanza kuhangaika huku na huku..
Ila nadhan ilikuwa hivo ili iwe funzo kwetu kuwa chemchem yako ipo, ila pengine Allah anataka aone juhudi zako na subra yako katika Kuitafuta..
‘Allah atupe Subra’
Maisha Ya Nabii Ibrahim, Alayh salaam..
Kupitia Hijja, tunajifunza maisha ya Nabii Ibrahim alayh salaam (yeye akiwa kama muasisi wa Al Kaaba) namna alivokuwa akiziendea amr za Allah..
Na hii ni kwamba alikuwa akitekeleza amr za Allah bila kusita wala kudelay, na wala alikuwa hauliz kwanin..
Mfano, alipoamrishwa amchinje mwanae Ismail, hakuuliza kwanin, ye alitii amr tu..
Pia alipoambiwa amuache mtoto wake na mkewe jangwan peke yao, hakusita, alitii amr..
Na kutokana na hilo, unapata funzo lingine hili hapa, kwamba..
Maisha si kwa ajili Yako
Kutokana na maisha ya Nabii Ibrahim, alayh salam unajifunza kuwa maisha si kwa ajili yako, Ila ni katika kumtii mola wako, Allah kwa utiifu wa juu zaidi..
Nabii Ibrahim aliamua kutoa kila kitu, na kujinyima kwa ajili ya Allah..
Allah anasema katika Qur'an..
{ قُلۡ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحۡيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ }
[Surah Al-Anʿām: 162]
Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na kuishi kwangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Allah, Mola Mlezi wa viumbe vyote..
Kwahivo, ukishajua hilo, ni kuweka matamanio yako kando kwanza, na kufanya yale ambayo tumeamrishwa tuyafanye kwakuwa maisha si kwa ajili yetu!
Experience Ya Siku ya Qiyama
Kupitia Hijja, tunaexperience siku ya Qiyama na hii ni kama dalili kwetu kuwa siku hio ipo..
Kwanza ukiangalia Aya za mwanzo za Suratul Hajj zinaongelea kuhusu Qiyama na Hali itakavokuwa siku hio..
Pia, watu kutoka mahali mbalimbali mwa Dunia, kukutana sehemu moja. Wote wakiwa katika Hali ya usawa — usiweze kumjua Tajiri, wala maskin— pia watu wenye backgrounds mbalimbali katika maisha yao, wengine wema, wengine wabaya. Woote wamekusanywa katika uwanja mmoja..
Hii ni dalili tosha kwetu kuwa, kama hilo limewezekana hapa Duniani, basi haliwezi kushindikana Akhera.
”Washuhudie Manufaa yao..”
Allah tabaraka wa taala anatueleza kuwa miongoni mwa Faida za Hajj, ni tushuhudie manufaa yetu..
Manufaa ya kushuhudiwa katika Hajj, ni mengi Ila mimi nitaongelea katika sehemu moja..
Kupata connection na network.
Hajj ni sehemu ambayo watu kutoka mataifa mbalimbali hukutana, ikiwa Lengo ni kwa ajili ya Ibada. Lakin pia ipo nafasi ya kujuana na watu, kufahamu maisha yao na stadi zao.
Na katika kuwafahamu huko unaweza pata network au connection yoyote ambayo inaweza ikakufaa katika maisha yako kidunia au kiakhera..
Mfano Rasulullah salallahu alayh wa salam, wakati anahitaji kuhama Makka. Alitafuta network hio kwa kukutana na makabila katika kipindi cha Hajj, AbuBakar Radhiyallahu anhu kama mtu aliekuwa akiyafahamu makabila alimtembeza na kumtambulisha kwa makabila hayo.
Ijapo wengi wao waliukataa ujumbe wa Uislam na wakamkataa Rasulullah, Ila hatimae watu wa Khazraj wakamkubali na tunajua baada ya hapo kuwa maisha ya Uislam yakabadilika..
Ilibidi iwe miongon mwa maajabu ya Dunia..
Ngoja nicheke kwanza..😄😄
Mi nadhani ilibidi iwe hivo. Maana hakuna mtu aweze kuikusanya Dunia nzima sehemu moja..😄
Na fikiria, ni Ibrahim alayh salaam ndie alietuita, lakini mpaka leo watu wanaitika “Labayka llahumma Labayk..” kana kwamba ametuita Jana. Allah Akbar!😄
Na licha ya tofauti zetu, Ila umoja wa pale ni wa kipekee. Ni miongoni mwa dalili kuwa wito huu unatoka kwa Allah, ambae ndie mwenye kuziunganisha nyoyo..
Na ni dalili kuwa hichi kitu si cha kutengenezwa na mwanadamu kama wengi wanavodhani, kwasababu kitu cha ukweli kutoka kwa Allah hubaki milele. Lakini cha mwanadamu hakiwezi baki milele..
Hivo Dunia inabidi ishuhudie ajabu hili..
Ni Mimi Mubaarak,
Shukran, Jazakallahu khayr!