Huu Ndio Ufunguo Wa Qur'an
Kama unataman uweze kuifungua Qur'an na Ikufae Maishani, basi soma hii mpaka mwisho..
Bismillah rRahman rRaheem
Assalam alaykum msomaji wangu mpendwa, karibu tena katika makala hii yako pendwa inayoandikwa na Mimi Akh. Mubaarak..
Kama ndio mara ya kwanza hapa, basi nikuombe usubscribe ili usikose Faida nyingi zijazo..
Shukran..
Utangulizi..
Ukweli ni kuwa..
Kila chumba cha thamani kinao ufunguo..
Kama vile ambavo unao ufunguo wa restroom yako ama ghetto lako, au ufunguo wa SAFE yako..
Na Qur'an kama kitu cha thamani, kinao ufunguo..
Kinao password, au niseme encryption keys..๐
Bila kuwa na huo ufunguo, hio password, au hio encryption key au vyovyote utavoiita huwezi kupata chochote cha kukunufaisha katika Qurโan..
Na kama ukiupoteza ufunguo huo hutoweza kupata uwezo wa kuifungua Qur'an na kufaidika, hivo Linda usiupoteze ufunguo huu nikishakuambia, In Shaa Allah..
Password Ni Hii..
Allah anatueleza ufunguo huu wa thamani katika aya hii..
{ ุฃูููููุง ููุชูุฏูุจููุฑูููู ุงููููุฑูุขูู ุฃูู ู ุนูููููฐ ูููููุจู ุฃูููููุงููููุง }
[Surah Muhammad: 24]
Mbona hawaizingatii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?
Katika Aya hii, Allah anakueleza kuwa..
Vipi?, Imekuaje? Huifungui Qur'an kwa "kuzitafakari" kisha kuzielewa, kuzifanyia kazi aya zake na kuzizingatia?
Kwahivo ufunguo wa Qur'an ni KUZITAFAKARI aya zake kisha kuchukua hatua stahiki juu ya kile ulichokielewa humo..
Na kupitia kuifungua Qur'an ndipo ambapo utapata hamu ya kufanya matendo mema, utapata hofu ya kufanya maovu, na utapata tumaini katika maisha yako na utatuzi wa shida zako..
Yani ni kama vile ambavo unafungua chumba chako ili ukapumzike, au ujistiri..
Au kama unavoweka password ya ATM yako ili utoe pesa. naam, namna hio..
Kufuli Za Qurโan..
Kama ambavo ipo Funguo inayokuwezesha kuielewa Qurโan na kunufaika, pia lipo Kufuli ambalo linafanya ukose kuielewa Qur'an na kunufaika..
Kufuli hizi zipo katika moyo, huufunga moyo usipate manufaa ya Qurโan..
Kufuli hizo ni kama vile Kibri, Majivuno, ujinga wa kuisoma Qurโan, kughafilika na kujisahau wajibu wako kama muislam, pia wivu..
Yani kiufupi, Yale maradhi ya Moyo, ni Kufuli zinazozuia usipate kufaidika na Qur'an..
Na hii ni kwamba unasikia amri katika Qur'an, katazo au funzo na we ukapuuza kutokana na Kibri, majivuno, au wivu na hivo vikawa ni Kufuli kwako.
Vimezuia usiipate faida ya Qur'an, na usiingize Nuru na uzuri katika Moyo wako..
Kwahivo, Funguo ya Qur'an itatumika kufungua makufuli haya..
Utakapokaa, ukiisoma Qur'an na kuzitafakari Aya zake, visa vyake, makatazo yake, Ahadi zake kwa waumini na hamasa yake..
Basi utafungua makufuli yote, na utakuwa mwepesi wa kufanya kheri, na amini Moyo wako utakuwa na Nuru..
Naam, hivo ilinde Funguo hii.. Yaani Isome na izingatie Qur'an. Maisha yako amini, hayatakuwa kama mwanzo..
Wabillah Tawfiq,
Allah akuhifadhi msomaji wangu. Na usinisahau katika dua zako..
Assalam alaykum
Al Akh Mubaarak!