Kanuni 1 Ya Muhimu Mno Katika Maisha..
Kama ningeifahamu na kuielewa kanuni hii mapema naamini nisingeumizwa na watu. Hivo soma hadi mwisho uifahamu mapema ndugu yangu..
Assalam alaykum..
Bismillah, Alhamdulillah wa salatu wa salaam alaa Rasulillah Salallahu alayh wa salam..
Karibu katika makala yako pendwa msomaji wangu, ni kwa mara nyingine Tunaenda kujifunza kitu kitakachotufaa katika Dunia yetu na Akhera yetu In shaa Allah..
Kama bado hujasubscribe, fanya hivo. Ili usikose faida tele zijazo..
Naam,
Tunafahamu kuwa Allah subhanahu wa taala, muweza wa kila kitu ameweka kutegemeana kwa viumbe katika kuishi kwao, inaitwa Ecosystem..
Na hii ipo kwa viumbe wote, tofauti zao, ndio kutegemeana kwao na kuishi kwao..
Vivo hivo na sie wanadamu kutofautiana kwetu katika kila Hali ndio UTAMU na kusudi la maisha lilipo..
Allah subhanahu wa taala anasema..
ۗ وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا
[Surah Al-Furqân: 20]
Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni majaribio, mitihan kwa wengine; je! Mtasubiri? Na Allah wako Mlezi ni Mwenye kuona..
Inaposemwa "tumejaalia baadhi yenu wawe mitihan kwa wengine" inamaanisha kuwa Allah amejaalia tofauti za watu flani ziwe mitihan kwa wengine..
Mfano Makuraysh wa Makka, miongon mwa sababu zilizowafanya wasisilimu licha ya kuusikia ukweli ni kwasababu Tu Rasulullah Salallahu alayh wa salam na masahaba zake wengi wao walikuwa ni masikini..
Kwahivo umaskini wa Masahaba ukawa Fitna, mtihan kwa Makuraysh..
Na hio ndio Fitna, ndio mtihan Allah katupa..
Kwamba mmoja ni Tajiri, mwingine ni masikini. Mmoja ana cheo mwingine Hana cheo. Mmoja ni kiongozi, mwngine anaongozwa. Mmoja ni bwana, mwingine ni kijakazi. Mmoja ana sura, muonekano mzuri mwingine Hana muonekano. Mmoja ana Mafanikio, mwingine Hana Mafanikio..
Mfano mtu anaweza ona fursa mahali flani, lakin kutokana na kuogopa watu, na akaajiuliza "watanionaje nikiwa nafanya kazi flani ya ajabu.." hivo mtu huyu akaacha kufanya kitu cha maendeleo kwa sababu ya watu fulani "WATAMUONAJE". Hivo hao watu wakawa ni mtihan kwake..
Ndo Allah katika muendelezo wa Aya anasema "Kwahio hamtasubiri?" Anauliza Allah. Kwahio utaacha kufanya la maendeleo ukiwaogopa watu watakuonaje?, Hutasubiri?, Ina maana achana na watu na fanya jambo la maana, kuwa na Subira kwa watakayo yasema..
Mfano mwingine, utajiri wa mtu unaweza kuwa mtihan kwa maskini. Hii ni kwamba kwasababu maskin nae anataman apate Mali sawa alizo nazo mtu fulan, au apate Mafanikio sawa na mtu fulan..
Hivo maskin huyu, au mtu huyu ambae hajafanikiwa akatafuta njia zisizosahihi, yaani njia alizozikataza Allah za kukusanya Mali yeye ndo akazifanya na hio ikawa ni mtihan kwake. Tajiri flan au mtu flan aliefanikiwa akawa ni mtihan kwa maskin huyu..
Sasa ndio Allah anamuuliza maskin huyu, "Hautasubiri?" Kwasababu sijakupa Mali ndo utaacha kusubiri na uhangaike kwenye haram. Yani Allah anamaanisha vuta subra..
Nikuongezee mfano mwingine, ni mwendo wa mifano Tu mpaka useme😄
Watu wawili waliokatika mahusiano, mfano mke na mume. Lazima kutakuwa na tofauti baina yao..
Yaani mume anapenda kitu flan, mke hakipendi. Au mke anapenda kitu flan mume hapendi. Au mume wako hayupo romantic lakin mume wa jiran Yako yupo romantic, au mke wako hajui kujali, mke wa jiran yako anajua kujali..
Na mifano mingine kama hio, Sasa kutokana na Hali hio mke au mume akaona bora amcheat Tu Mkewe au mumewe ili kufidia hizo gapes, ndo Allah anamuuliza mwenza wa namna hii "Kwahio Hautasubiri?" Kwasababu mumeo/mkeo sio romantic, kwasababu mumeo hana hela ndo umfanyie khiyana?. Yaani Allah anamaanisha "Kuwa na Subra"
Au mtu, mume/mke, kutokana na tofauti hizo asizozipenda kwa mwenza wake ikapelekea kumtreat vibaya mwenza wake na kumtolea maneno machafu. Na ikapelekea mtu kukosa Thawabu na akaingia makosan kwasababu ya mtu fulan kuwa mtihan kwake na akasahau kusubiri..
Mfano mwingine pia ni watoto, watoto wanaweza kuwa mtihan kwetu kwa wewe kushindwa kuwalea, au wanafanya usioyapenda. Hivo Allah anauliza "Kwahio utaacha kusubiri?" Utaacha kusubiri na kuvumilia katika kuwalea na kuwaongoza?
Hivo vumilia, waeleze, walee na umuombe Allah kwa msaada..
All in All ni kwamba kila mtu unaekutana nae, MTU YOYOTE alie mbele yako, unaeamiliana nae, unaefanya nae kazi, ambae upo katika mahusiano nae huyo ni mtihan kwako kwa namna yoyote. Hivo mvutie subra, mvumilie katika Yale ambayo unaona yanakukera kutoka kwake na umuombee dua..
Na mtihan huu unakuja pale ambapo, kwasababu yao watu tunamkosea Allah, tunaacha kufanya ya maendeleo, tunawakosea wengine n.k..
Au iga mfano huu wa Abu Hurayra..
Wakati wowote Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) alipoona kampani ya mtu, ( au kuamiliana) na mtu ni uzito juu yake, alikuwa akisema:
" اللهمَّ اغفر له وأرِحنا منه "
“Ee Allah msamehe na utuepushe naye.”
[Ibn Qutaybah (rahimahullah) katika ‘Uyoon al-Akhbaar, 1/279]
Na kama Allah alivotuelekeza, ukiona mitihan imekuzonga, Call 911😄. Yaani ongea na Allah kama Allah anavosema..
{ وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ }
[Surah Al-Baqarah: 45]
Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu..
Naam, namna hio Akhy/ ukhty yangu, Sala na Subra, Dua na Subra. Ya watu hayaishi, maneno, kukera hakuishi..
Na hio ndio kanuni moja ya muhimu mno ili uweze kuishi na watu, wavumilie, kuwa na Subra na Allah anaona, kama Aya inavomalizia ( Na Allah wako Mlezi ni Mwenye kuona..) na atakulipa ujira wako ima iwe hapahapa dunian, au kesho Akhera, In shaa Allah!.
Usinisahau katika dua zako ndugu,
Ni Mimi Al Akh Mubaarak,
Assalam alaykum..
Kwa ushauri, maoni, na ukumbusho, nichek Whatsapp