Ukiachana na hilo kuwa mziki una athari juu ya Iman yako na unakuweka mbali na Qur'an na Dhikr..
Lakin pia mziki una athari kwako kama hiz zifuatazo.
Katika Uislam na Sayansi, Mziki una athari sawa na Pombe, Zinaa na kamari..
Hii ni kwasababu, katika sayansi inaelezea kuwa vitu vyote hivo(pombe, zinaa, na mziki) huenda kureact katika Limbic System kwenye ubongo
Na kutokana na athari zake kwenye limbic system, mziki huathiri akili na hisia zako sawa na pombe, ngono na kamari. Na kukufanya uwe tegemez (addiction) na kuathiri namna unaamua mambo..
Na pengine ndo maana mtume Salallahu alayh wa salam alivitaja hivyo vyote katika sentensi moja, pale aliposema..
لَيَكُونَنَّ مِنْ أُمَّتِي أَقْوَامٌ يَسْتَحِلُّونَ الْحِرَ وَالْحَرِيرَ وَالْخَمْرَ وَالْمَعَازِفَ،
“Miongoni mwa ummah wangu kutakuwa na baadhi ya watu watakaofanya zinaa, uvaaji wa hariri, unywaji wa pombe na utumiaji wa vyombo vya muziki kuwa ni halali..”
Sahih al-Bukhari 5590
Mziki hukubadilisha tabia kutokana na mashairi, Lyrics zake.
Maneno ya wimbo yanaweza kusukuma fikra na matendo yasiyofaa kiimani. Kwakuwa huingia moja kwa moja moyon. zikikufundisha kupenda haram, maasia, na kujiona huru bila mipaka ya dini..
Mziki huteka hisia zako na namna unafanya maamuzi.
Midundo na sauti za muziki, huteka emotions na kuathiri jinsi unavyofikiria, unavyohisi, hadi unavyohukumu mambo ya maisha.
Hukuwekea unafik katika moyo wako juu ya imani yako kwa Allah.
Unapovutiwa na muziki kupita kiasi, moyo unavurugika katika kuheshimu Amri za Allah na badala yake unafanya yale ambayo moyo hutamani.
Na hii ni kwakuwa unaweza vipi kupenda Qur’an na wakati huo huo kusikiliza nyimbo zinazopingana na mafundisho yake?
Hukusahaulisha wewe ni nani na upo duniani kwa ajili gani
Mziki hukufanya uzame katika burudani hadi kusahau malengo yako kuwa upo kwa ajili ya ibada..
Nikimalizia kwa kauli ya ulamaa..
AdDahaaq anasema “Muziki na kuimba husababisha upotevu wa mali, kupata hasira za Allah na kuharibika moyo”
[Ibn al-Jawzi, Talbees Iblees.]
Kwahio, Hii ni nafasi yako kutafakari: Je, muziki unakujenga au unakuondoa kwa Allah??
Ni Mimi ndugu yako Mubaarak,
Assalam alaykum..
Share this post