Passkeys 5 Za Siri Za Swaumu (Funga)
Passkeys 5 ambazo utaweza kufungulia ufahamu juu ya Faida ya Funga maishani mwako..
Nimeitizama swaum hii kitofauti, Alhamdulillah, nikaona vitu ambavyo. Naamin vitakufaa maishani. Na vitakusaidia na wee uitizame swaum kitofauti pia..
Pengine unaichukulia kufunga kama kufunga tu, yan kama Ibada tu. Lakin kwa uwezo wa Allah nilikuja kuona kuwa kuna kitu tunafundishwa hapa, Sisi kama waislam, waumini..
Na kiukweli ukinielewa katika haya nitayokuambia, naamin utaelewa SIRI ziliopo ndani ya kufunga..
Yaani kila stage ina SIRI yake, kuanzia kufunga mchana, kufutari jioni, hadi daku..
Na nikaona SIRI hizi 5, wacha nishee(share) na wee ndugu yangu, mwanangu sana!😁
Biidhnillah, asaa itakufaa..
SIRI #1: "NIA" ya Swaum, Usitoke nje ya lengo..
Kila siku unaweka Nia hii kwamba "Kesho Biidhnillah, Nitafunga kwa ajili ya Allah.."
Na Nia hii Ipo katika Ibada zote. Kila kitendo huangaliwa NIA..
Lakin issue ni kwamba NIA hii inatakiwa iwe updated kila mara ili kujihakikishia usalama wa Ibada yako hio..
Kwasababu inaweza tokea ukaanza na Nia nzuri ya kufanya Ibada kwa Allah, alafu mwishon ikatokea mauzauza, Riyaa ikakupitia basi, ukawa umefanya Ibada kwa ajili ya watu..
Mfano, unaweza ukawa umefunga, lakin kutamka kwa kila mtu "mi nimefunga, mi nimefunga.." bila ya haja maalum. Hili linaweza likafungua Mlango wa Riyaa, kwamba watu wakuone we ni mfungaji..
Ukawa umeshinda njaa na pengine malipo usiyapate..
Hio ni katika Swaum, lakin hilo la NIA tunalipata katika Ibada zote. Hivo ibada yoyote unayofanya kwa ajili ya Allah ihakikishe Nia yako isitoke nje ya lengo..
SIRI #2: Kufunga Mchana, Ni Kipimo Cha Subra..
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Kufunga ni nusu ya subira."
Imepokewa na At-Tirmidhiy.
Subira ipo katika aina tatu: subira katika kumtii Mwenyezi Mungu, subira ya kujiepusha na yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, na subira ya kukubali amri ya Mwenyezi Mungu inapoumiza. Aina zote tatu za subira zimeunganishwa katika kufunga.”
(Lataa’if al-Ma‘aarif cha Ibn Rajab, uk. 150)
Na hapa nitashuka kwa vipengele..
A. Njaa inatesa, njaa inauma sio poa. Ila swali ni kuwa nani unaelekea kucomplain maumivu yako?
Na hicho ni miongoni mwa vielelezo vya Subra, unapopatwa na shida, dhiki maumivu, usianze na yoyote kabla ya Allah..
Kama alivosema Yaaqub(a.s)
{ قَالَ إِنَّمَآ أَشۡكُواْ بَثِّي وَحُزۡنِيٓ إِلَى ٱللَّهِ }
[Surah Yūsuf: 86]
Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu.
Kwahivo wakati swaum imekaza hasa, hapo ndo wakati mzuri wa kumkumbuka Allah..
Na katika maisha yako unapopatwa na shida, basi uanze na kumuomba msaada Allah kwanza kisha ndo uangalie raman zingine..
B. Unaoneshwa kuwa maisha haya ni kusubiri juu ya dhiki za muda mfupi, kama ambavo unasubiri juu ya dhiki ya Swaum ndani ya masaa 12 ya mchana..
Hivo usije ukakosa Subira katika maisha haya, jua kuwa shida unazozipata ni Swaum. Na futari yake ipo siku moja, Jannah, In Shaa Allah..
SIRI #3: Wakati wa kufutari, Pata Pesa(Neema) tujue Tabia yako..😄
Huo msemo ni common sana, Pata pesa tujue Tabia yako..
Sasa mi nasema, Tabia yako tutaijua wakati wa kufutari. Unajua kivipi..
Wakati ule ni wakati wa Neema, Yan ni sawa umehustle alafu michongo ikatick, vibunda(pesa) vya kutosha..
Sasa kama wewe ni mbakhili tutajua, kama upo humble in nature, tutajua, kama unapenda kusaidia walio chini tutajua..
Kwahio wakati wa kufturu mtu unajipakulia minyama na hujali, basi huenda hata ukijipata kifedha hutajali mtu..
Kama wakati wa kufturu humkumbuki maskin, hujawahi lisha hata mtu moja, hujawahi saidia hata kumfuturisha rafik yako. Pengine hata ukijipata kiuchumi utakuwa Hivo hivo..
Na wakati wa kufturu kama wewe ni mtu wa israaf tutajua. Utataka ule kila kitu na huwezi, mwishoe utamwaga chakula..
Na ndio hata ukipata pesa pengine utakuwa hivohivo utaitumia vibaya..
Mtume s.a.w anasema
“Sisi kundi la manabii, hatulii mpaka tusikie njaa, na tukila hatuli tukashiba”
Na ndio maana Rasulullah s.a.w akatuusia sana tulishe maskin, tufuturishe, hii ni ili kutujenga kuwa hata pale wakati Allah atakapotuneemesha tusiwasahau wengine..
SIRI #4: Baada Ya Kuftari; Je, unazishukuru Neema za Allah..
Mzee mwenzangu ndo ushashiba sasa, kitumbo ndii, shibe mwana malevya..😄
Hapo ndo inabidi unyanyuke ukaswali TARAWEEH..
Kama kweli unamshukuru Allah kwa alichokuruzuku ukala ukashiba basi hutoona uzito kuamka kwenda Taraweeh na kufanya Ibada zingine..
Na inaonesha kuwa unajali kile ambacho amekuruzuku Allah, na unamshukuru kwa alichokupa hivo unafanya Ibada kama miongoni mwa njia za kuonesha shukrani yako kwake..
Lakin kama we huzishukuru Neema za Allah, Basi utaendelea na mambo yako. Siku ndo ishaisha hio..
SIRI #5; Daku, Mida Ya appointment na Baraka za kushato(kutosha)..
Kitu nilifikiri kuhusu Sunnah ya daku kuwekwa karibu na alfajir ni kuwa pengine Allah anatuandaa tuzoee kuamka mida hio kwasababu..
Kwanza ni mida ya Appointment, mi naiita Tahajjud ni appointment, ndo mida ambayo Allah hushuka kwa dhati yake na kumsikiliza anaemuomba..
Hivo Allah, kwa rehma zake anatuzoesha tuweze kuamka na kumuomba yeye katika mida hio..
Pili, Ni mida yenye Baraka, Kama alivoomba dua Rasulullah s.a.w kwamba "Ubariki Umma wangu, kwa wale wenye kuamka mida ya alfajiri” na katika hadith nyingine, "Kuleni daku, kwani hakika kwenye daku kuna baraka”
Kwahivo tunaona ni mida ambayo imebarikiwa kwa kiasi kikubwa. Hivo, jambo lolote utalofanya kwenye mida hio lazima, Biidhnillah litazaa matunda mengi mazuri..
ni mida iliotulia, kamaukisoma vitu vinaingia, na kama ukifanya kazi zako mida hio, kazi zinaenda smoothly, kiulainii..
Hivo, tujitaahid kuamka kula Daku, kwa Sunnah. Kuanzia saa 9 hivi hadi 11 kasoro hivi..
Mi nimemaliza kukumwagia siri mwanangu wa nguvu, ndugu yangu..
Bye, siku nyingine In Shaa Allah..
Mubaarak
WhatsApp : 0686011682
Au click hio link “WhatsApp”