Safari Yangu Na Qur'an
Ilikuwa Mwaka Jana, 2024. Nilipoamua Kusafiri Na Qur'an. Na Huu Ndio UKWELI wa Qur'an Niliougundua Kwenye Safari Hio..
Ilikuwa mwaka Jana, 2024. Nilipoanza safari yangu ya kuamua kuisoma Qur’an kila siku, na kwa uwezo wa Allah Alhamdulillah si haba..
Ijapo ilikuwa ngumu siku za mwanzo, ngumu sana tena. Ila nilijitaahid nisikose hata nusu karatas tu..
Na katika safari hio, niligundua UKWELI huu kuhusu Qur’an..
Naamin mambo haya matano (5) ya kweli yata blow your mind wanasema kwa kimombo..😄
Shuka nami👇🏼
1. Qur'an, haipendek hivi hivi tu..😍
Yahitaji kubembelezwa. Na uoneshe kuwa unaihitaji..
Namaanisha kuwa, kwa siku za mwanzo hutoona utamu wa kuisoma Qur'an, wala hutoona hamu ya kuisikiliza mara kwa mara, muda wote..
Ila mpaka pale utakapoamua kuwa king'ang'aniz na uoneshe kuwa unahitaji uipende.
Na hii ni pale ambapo huna hamu ya kuisoma ila unajitahid uisome, unasoma kidogo umechoka, Ila unajilazimisha uongeze hata karatas moja, huna hamu ya kuisikiliza Ila unajitahid uisikilize..
namna hio..
Kisha ndo utaona Allah atayatia mapenz ya Qur'an katika?? moyo wako, na utapenda zaidi uisome, uisikilize na ujue maana yake..
2. Qur'an ina wivu😄
Nimetumia neno hilo ili unielewe vizuri..
Na wivu wake ni kuwa, Huwez ukapenda Mziki au chochote cha ajabu pamoja na Qur'an.
Qur'an automatically itaondoka. Inakuacha na ukipendacho. Kile ambacho kinakulia muda wako. Kama mziki, social media, kuchat e.t.c au ukawa busy na kazi zako siku nzima bila kuitengea muda Qur’an. Basi mapenz na Quran yanapungua..
3. Qur'an haikawii kukusahau..
Qur'an ukiisahau, usiipitie kila siku. Ukaanza kuipuuza. Nayo utaona kabisa, inakupotea na mapenz yanapungua. Inaondoka kabisa katika moyo wako..
Chukulia uwe na rafiki yako mlieshibana sana na itokee msitafutane kwa mwez mzima au miez kadhaa. Hapo lazima urafiki wenu utakuwa ushaanza kuwa na shida mahali.. na Qur'an ni hivohivo..
4. Qur'an ukiipenda ile kuipenda kihakika inakuwa rafiki yako..👥
Na itakupa utatuzi wa shida zako, itakupa subra, matumaini na amani. Na huenda hata kukubadilisha Tabia na kukuchagulia marafiki. Hii ni kama maajabu flan hivi..😃
5. Qur'an huongea na watu wake..🗣️
Na inaweza kujibu mashaka yako yaliyomo nafsini mwako au kukupa amani kutokana na hofu uliyonayo..
Yani hii inatokea pale ambapo, hujui nini cha kufanya kuhusu jambo linalokusibu au unalopitia..
Sasa, kwakuwa Qur’an ni rafiki yako na haipiti siku bila kuisoma. Utagundua katika hicho utachokisoma utapata utatuzi wa kile kinachokusibu..
Yani ni kama maajabu..🙂
Sasa ili unielewe vizuri kwenye hio point ya mwisho sikiliza hiki kipande cha interview cha Sheikh Fadel Suleman, Mfasiri wa Qur’an huyu na mkufunzi akiwa anahojiwa na Toward Eternity..
Anaeleza namna Qur’an huongea na watu wake kwa mifano halisi. Click YouTube
Mpaka hapo, sina la ziada. Nishakumwagia ukweli. Ni ushindwe wewe tu..
Shukran, Assalam alaykum.
Mubaarak!