Surat Yusuf Na Mchoro Wa Ramani Ya Mafanikio..🗺️
Ikiwa unahitaji kufanikiwa katika maisha yako, soma hii, nikuelezee vituo tisa (9) vya kuvizingatia katika ramani yako ya Mafanikio.. Shuka nami👇🏼
Bismillah..
Assalam alaykum warahmatullah..
Mambo vipi?, Karibu tena katika makala yako pendwa kutoka Ahadun Ahad Studio..
Inayoandikwa na mimi Akh. Mubaarak.
Kabla sijaendelea kukuelezea kituo kimoja baada ya kingine katika ramani hii Adhwim inayopatikana katika Surat Yusuf..
Basi nikuombe usubscribe ili usikose kheri nyingi zijazo..🙂
Shukran..
Utangulizi..
Naam..
Wacha tuendelee kama ifuatavyo Akhy /ukhty yangu..
Ukweli ni kuwa kila mtu anahitaji kufanikiwa katika shughuli zake, biashara zake..
Kufanikiwa katika mishe zake, michongo yake, hustle zake, madusko yake katika kuzingatia kwake maokoto..😄
Eee vijana tuna msamiati mingi..😄
🙌🏼
Sasa katika hustle kama hio, ni ngumu sana kutoboa ( Kufanikiwa) kama huna roadmap, kama huna blueprint ya kukuongoza..
Na katika hilo kila mtu anapo ambapo huchukua maelekezo na guidelines zake katika mapambano yake, na majibu yake kuhusu maisha..
Sasa wewe kama Muislam, hakika hukuachwa bure katika maisha haya, Ila ulipewa muongozo juu ya maisha, Ibada, miamala yako na hata mahusiano yako na watu..
Sasa kuhusu kuhaso(hustling), Tunaupata muongozo wake katika Surat Yusuf..
Kwanini Surat Yusuf..
Zipo sababu nyingi zilizofanya niichague Surat Yusuf kuwa kama guideline juu ya maisha yako na Mafanikio yake. Ila nitakupa points mbili nzito alizozieleza Allah mwenyewe..
Moja, Allah mwenyew anaiongelea Surat Yusuf kama "ahsanul qasas" yaani "kisa kizuri" na miongoni mwa sababu za kuitwa hivo ni kuwa inamgusa kila mtu kwa sifa yake na nafasi yake na kumuonesha vipi aishi na vipi afanye ili afanikiwe..
Na hii ni muhimu mno kwa vijana, vijana sie ndo ambao tunahamu zaidi ya Mafanikio, tunahamu zaidi ya kufika mbali, ikiwezekana tufike haraka..
Pili, vijana sie tuna maswali mengi mno tunajiuliza kichwani, maswali ambayo hatuyapatii majibu yake..
Na ndo utasikia wengi wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo, kujinyonga, kuingia katika makundi maovu, madawa ya kulevya na mengi katika maovu ni sie vijana..
Siku moja nilikuwa nasikiliza Podcast ya SalamaNa..
Salama alikuwa akimuhoji Mchungaji Hananja, ambae ukiachana na kazi yake ya uchungaji pia ana sober house, Ile nyumba hupelekwa waliokuwa addicted na madawa ya kulevya..
Na katika kuhojiwa alisema..
"vijana wengi hufikia katika hatua hio ya madawa na msongo wa mawazo kwasababu wamekosa Majibu ya maswali yao kuhusu maisha.."
Sasa Surah hii ni majibu ya maswali yako kuhusu maisha, yaani ni full answer sheet..🙂
kama Allah anavosema..
{ لَقَدْ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِ آيَاتٌ لِلسَّائِلِينَ }
[Surah Yûsuf: 7]
Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara(majibu) kwa wanaouliza..
Nianze kukuchorea ramani..🙂
Sasa basi nini tunajifunza katika Sura hii yenye kisa kizuri ili iwe kama ramani katika Mafanikio yako..
Ramani hii nitaichora kwa kukuelezea vituo kwa mujibu wa mtiririko wa aya zilivojipanga..
Ikiwezekana kaa chini usichoke maana, hii ramani ni ya mjengo mkubwa sana na ina vituo vya kutosha, Ila Leo nikupa vituo vikuu Tisa(9)..😄
Naomba uwe makini, ninapoipitisha penseli yangu nawe ufuatishe..
Hii ni ramani muhimu sana..🙂
Kituo 1; Ndoto Zako, Zifiche..
Huwa tuna ule msemo tunasemaga "Babu yangu aliiniambia.."😄, au "baba yangu alinihusia.."
Sasa na sie tulihusiwa na Babu yetu Yaaqub.. alitupa usia kuwa..
{ قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنْسَانِ عَدُوٌّ مُبِينٌ }
[Surah Yûsuf: 5]
Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.
Kila mtu anazo ndoto, wachana hizi za Kuota usingizini..😄
Ila unazo ndoto zako juu ya maisha yako, na Biashara zako.
Pia unazo Neema ambazo Allah amekupa ambazo hizo Neema zako ni ndoto ya wengine..
Sasa babu anatuusia usisimulie ndoto zako za maisha yako HOVYO kwa nduguzo, jamaa n marafiki, na pia usipende kutangaza Neema zako, jitaahid sana kuuchunga ulimi..
Kwanini?, Kwasababu vitimbi vitafuata, wanaweza wakuwekee vikwazo katika mishe zako, na michongo kwasababu ya Husda..
Lakin babu akamalizia kwa kusema "Hakika ya Shaytwan ni adui aliedhahiri.."
Kumaanisha kwamba si wao nduguzo Bali ni shetan ndo hutia wasiwasi katika masikio yao ili wakufanyie Husda wewe..
Kituo 2; Shida Ni Wewe, Si Wengine..
Yani usitafute Excuses za kutokufanikiwa kwako kupitia mtu mwingine, au kitu..
Pia usitafute attention kwa mkubwa wako, au yeyote aliejuu yako kupitia kumuumiza mwingine, usiwe mbinafsi..
Na angle hii ya mchoro tunaisoma katika Aya, Allah anapotueleza..
{ إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ }
[Surah Yûsuf: 8]
Pale walipo sema (nduguze Yusuf) Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, hali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotofu wa dhaahiri..
{ اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا مِنْ بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ }
[Surah Yûsuf: 9]
Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi mbali ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi. Na baada ya haya mtakuwa watu wema..
Ndugu zake Yusuf, hawakuwa watiifu kwa baba yao na walikuwa na kiburi kutokana na nguvu zao..
Lakini hawakuona shida hizo kuwa ndo zinazofanya wasipendwe bali wakaleta sababu kuwa Yusuf ndio kizuizi cha wao kupendwa na Baba yao..
Hawakufanya Juhudi zozote katika kumtii Baba yao na kumheshimu wala hawakuangalia makosa yao..
Kwa hivo, katika kutafuta mafanikio usipende kuwapa watu kuwa ndo sababu ya kutokufanikiwa kwako, Bali jitathmini mwenyew una shida gani kisha jirekebishe..
Kituo cha 3; Subira Njema..
Katika kutafuta kwako, utakutana na watu wa aina mbalimbali, watakao kupenda, na watakao kuchukia..
Ukiwapata watakao kupenda na kukusaidia katika maisha yako ya hapa na pale hio itakuwa kheri kwako. Na itapendeza ukiwafanyia wema kama watakao kufanyia..
Ila ukiwapata wanakuchukia, wale tunawaita Haters!, Masnitch!.😄
Yani wale ambao hufanya mambo yako yasiende poa. Either kwa maneno Yao au kwa vitendo vyao. Basi cha kufanya wewe ni Subira Njema..
Tumuige babu yetu Yaaqub. Yaaqub wanae wakubwa, ambao kwa namna moja au nyingine ni Haters waliamua kumfanyia vibaya Yusuf na hilo lilimuumiza mno Mzee Yaaqub. Lakini aliwajibu vipi..
{فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَاللَّهُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ }
[Surah Yûsuf: 18]
Lakini subira ni njema; na Allah ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza.
Kwahivo katika safari yako ya Mafanikio ukikutana na haters, usitake kupigana nao, Bali lazimiana na Subra na umuombe Allah akusaidie juu yao..
Kituo cha 4; Mtu Si Nyau😄
Kauli hii niliisikia kwa rafiki yangu flani, maana yake ni kuwa mtu yoyote unaekutana nae usimpuuze..
Bali jitaahid kumjua vizuri huenda ukapata kitu kitakachokufaidisha kutoka kwake..
Tusiwe kama ule msafara wa biashara, waliomtoa Yusuf kisimani, na hawakumuuliza hata jina, wala anaishi wapi, wala kaingiaje kisimani, na wala hawakutaka kujua chochote kuhusu yeye..
Ndo kwaaanza wakamficha, Wakamfanya dili..😄, kumuuza Misri tena kwa bei chee. Subhanallah!😄
Pia katika maisha si kila unaekutana nae atajali kuhusu wewe, wengine hujijali wao zaidi na hukutumia wewe kwa manufaa yao. Hivo jitaahid ujue hilo..
Allah anasema..
{ وَشَرَوْهُ بِثَمَنٍ بَخْسٍ دَرَاهِمَ مَعْدُودَةٍ وَكَانُوا فِيهِ مِنَ الزَّاهِدِينَ }
[Surah Yûsuf: 20]
Na wakamuuza kwa thamani duni, kwa dirham chache mno. Wala hawakuwa na haja naye..
Kituo cha 5; Wema Hauozi..
Katika safari yako ya Mafanikio, utakutana na watu mbalimbali, wakirimu vizuri, ishi nao kwa wema, watunze. Hakika watakufaa baadae..
Haijalishi ni wenye vyeo vya chini zaidi na umewazidi katika baadhi ya vitu, wafanyie wema. Wema hauozi..
Na hilo alilifahamu aliemnunua Yusuf, ambae alikuwa ni waziri wa uchumi. Licha ya kuwa aliemnunua Yusuf kama mtumwa ila alimkirimu kama mwanae, akiamini wema hauozi..
{ وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِنْ مِصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ أَنْ يَنْفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ }
[Surah Yûsuf: 21]
Na yule aliye mnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makaazi ya hishima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwenetu.
Kituo cha 6; Comfort Zone..
Inasemekana mtu hawezi fanikiwa akiwa kwenye comfort zone..
Comfort zone, ni Ile Hali ya ukawaida wa maisha, huna changamoto yoyote umeridhika na jinsi maisha yalivo..
Ili mtu afanikiwe inabidi apitie changamoto na misukosuko. Na asipotaka misukosuko ya maisha yampate akaridhika, basi yeye si hustler, ni ngumu mno kutoboa(Kufanikiwa)
Hivo Allah alimtoa Yusuf kwao kwenye comfort zone ya baba ake akampitisha kwenye hali zote hizo hadi kufika Misri kwakuwa Allah alitaka Yusuf afanikiwe juu ya ndoto yake..
Hivo na wewe ukitaka ufanikiwe, jitoe katika comfort zone yako..🙂
Allah anasema..
وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِنْ تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
[Surah Yûsuf: 21]
Na kama hivyo(kumtoa Yusuf Madyan Hadi Misri) tulimweka Yusuf katika nchi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Allah ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui..
Pia stick to the Allah's plan ( mtegemee Allah juu ya plan zake) muamini Allah katika kila anapokupitisha, subiri Subra njema, hakika wewe ni Yusuf kwake na atakufikisha katika ndoto zako..
Kituo cha 7; Jihadhari Na Dhulma..
Katika safari hii ya kupambana na kutafuta, basi Jihadhari na Dhulma, na kuiba au kula Mali ambayo si halali kwako..
Hii inaweza kuwa Mali ya boss wako, au Mali ya ofisi au sehemu yoyote ambayo umeachiwa kama amana..
Na huenda ukaona kuwa ukifanya hivo unamdhuru yule unaemdhulumu pekee lakini kiuhalisia unamkosea hata Allah aliekuweka katika kazi hio au ofisi hio..
Tunajifunza hili kupitia Yusuf ambae licha ya kuwa mke wa waziri alimuita kimatamanio lakini hakufanya kile alichoitiwa kwasababu alielewa kuwa ni dhulma kula Mali ambayo si halali kwake..
Kula Mali ambayo yeye amechiwa kama amana, na pia ni kumkosea Allah ambae amempitisha katika shida zote hizo na kumsaidia..
Na wenye kufanya Dhulma hawatoboi..
Allah anasema..
{ ۚ قَالَ مَعَاذَ اللَّهِ ۖ إِنَّهُ رَبِّي أَحْسَنَ مَثْوَايَ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ }
[Surah Yûsuf: 23]
Audhubillahi! Najikinga na Allah.. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye kudhulumu hawafaulu..
Kituo cha 8; Mtegemee Allah Pekee..
Katika Hali yoyote utakayokutana nayo katika kutafuta kwako basi mtegemee Allah..
Fahamu kuwa yeye ndie aliekuweka katika Hali hio na yeye ndie atakaekutoa. Haijalishi upo katika Hali nzuri au mbaya..
Ikiwa upo katika Hali mbaya kumbuka alikupitisha katika Hali nzuri na yeye ndie atakae kurudisha huko..
Ikiwa upo katika Hali nzuri, basi zidisha kumshukuru na kumkumbuka yeye..
Yusuf alisahau kuwa Allah ndie alimtoa kwako Madyan, akamleta Misri, akamkuza katika nyumba ya waziri na ndie aliekadiria yeye akafungwa na yeye Allah ndie atakae mtoa jela..
Allah anatuambia kuwa shaitwan alimsahaulisha. Hivo nawe usijekusahaulishwa na shaitwan kuhusu kumtegemea Allah..
{ وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُ نَاجٍ مِنْهُمَا اذْكُرْنِي عِنْدَ رَبِّكَ فَأَنْسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ }
[Surah Yûsuf: 42]
Na akamwambia yule aliye jua kuwa atatoka (gerezani) katika wale wawili: Nikumbuke kwa bwana wako. Lakini Shet'ani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa..
Kituo Cha 9; Bila Kuchoka..
Nikumalizie kituo cha mwisho kwa wosia wa Mzee Yaaqub kama tulivoanza..😄
Mzee Yaaqub anakuambia katika kutafuta kwako usichoke, usikate Tamaa, “never give up”, “never settle” tunasema..😄
Yaani usipoteze tumaini na Allah atajaalia siku moja kila kitu kitafunguka na utapata unachokihitaji..
{ يَا بَنِيَّ اذْهَبُوا فَتَحَسَّسُوا مِنْ يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَيْأَسُوا مِنْ رَوْحِ اللَّهِ ۖ إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِنْ رَوْحِ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ }
[Surah Yûsuf: 87]
Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraji ya Allah. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Allah isipo kuwa watu makafiri..
Nimalizie..
Sina cha kumalizia Ila kama Surat Yusuf yenyewe inavomalizia kwa maneno yake kuwa..
{ لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ۗ }
[Surah Yûsuf: 111]
Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili..
Hivo ramani hii nimeimaliza na vituo vyake, lakin amini kuwa Surah hii na nyingine nyingi zina mambo mengi mno ya kujifunza..
Hivo ukiishika Qur’an hakika utafanikiwa..
Sina mengi, hata hivo nikupongeze kwa kumaliza vituo vyote Tisa(9), wallah si rahisi..🙂
Ni Mimi Al Akh. Mubaarak..
Ahadun Ahad Studio..
Assalam alaykum..🤗
Usisahau kusubscribe kwa mengine mengi yajayo..
Ikiwa una maoni, ushauri, swali, au unataka kutoa Sadaka yako juu ya kuendeleza kheri hii, basi nitafute kwa WhatsApp, click hapo chini..