Tahadhari Usijidhulumu Tena.
Umekuwa Ukijidhulumu Kwa Muda Sasa, Ikiwa hujui kivipi, Basi Soma Hii Mpaka Mwisho.
Huenda umeshtushwa na kichwa cha habari cha makala hii, na ukahitaji kufahamu ni kivipi unajidhulumu mwenyewe.
Basi wala usijali. Ndani ya dakika 3 zijazo utapata kufahamu ni kivipi unajidhulumu mwenyewe na jinsi ya kujitoa katika dhulma hio.
Lakini kabla sijaendelea, nikukumbushe kitu akhy/ukhty. Ikiwa bado hujasubscribe, tafadhali fanya hivo ndugu. Hii itakusaidia wewe usiweze kukosa faida na makala nyingine nzuri kutoka kwangu.
Ni rahisi tu, Weka email yako hapo chini, kisha bonyeza subscribe.
Haya, Tayari akhy/ukhti?, Sawa, wacha tuendelee.
Ukweli ni kwamba akhy/ukhty yangu kinachofanya unaidhulumu nafsi yako si kingine bali ni Kutokuifahamu na Kutoiheshimu miezi mitukufu.
Ndio, Miezi Mitukufu. Miezi mitukufu ni miezi iliopo katika kalenda ya kiislamu ambayo muislam unaifuata katika kutekeleza Ibada zako kama vile Hajj na kufunga Swaumu ya Ramadhani.
Miezi hio mitukufu ipo minne ambayo ni Dhul Qa’ada, Dhul Hijja, Muharraam na Rajab. Au unaweza kusema mwezi wa 11, wa 12, wa kwanza na mwezi wa 7 katika mpangilio wa miezi 12 katika Kalenda ya Hijri.
Miezi Hii Imekuwaje Mitukufu?
Sasa akhy au ukhty yangu msomi, kabla sijakueleza namna unaweza itoa nafsi yako katika dhulma. wacha nikueleze utukufu wa miezi hii umekujaje.
Utukufu wa miezi hii umekuja pale Allah aliposema
{ إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِنْدَ اللَّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنْفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ }
[Surah At-Tawbah: 36]
Hakika idadi ya miezi kwa Allah ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Allah ttangu alipo umeba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamungu.
Katika Aya hio tunaona vile Allah ametueleza kuhusu miez minne mitukufu na kwamba tusidhulumu nafsi zetu humo.
Allah ameitukuza miezi hii minne juu ya miezi mingine kwakuwa amekataza ndani ya miezi hii kufanya maasia, pia akaamrisha ndani yake Ibada na kujituma katika kheri na akaahidi ujira maradufu kwa watakaofanya kheri katika miezi hii.
Na hakika, atakuwa amejidhulumu yule ambae atakuwa hajatekeleza kheri nyingi katika miezi hii na yule ambae atakaechuma madhambi katika miezi hii.
"Dhulma katika Miezi Mitukufu ni mbaya zaidi na haependezi zaidi kuliko dhulma katika miezi mingine. Hakika dhulma ni dhulma siku zote, lakini Allah huyafanya mambo kuwa makubwa kuliko mengine atakavyo..” - Qatadah, Tafsir Ibn Katheer.
Cha Kufanya Ili Kujitoa Katika Dhulma.
Kama tulivoona utukufu wa miezi hio minne na kukatazwa kufanya dhulma katika miezi hio. Basi tufanye yafuatayo ili tuepuke kujidhulumu.
Inapaswa kuheshimiwa na kuchukuliwa kuwa ni miezi mitukufu
Tekeleza Amri za Allah kwa qadar ya uwezo na jitihada zako.
Tekeleza ibada za Faradhi kikamilifu
Jitahidi kujiepushia na Maasia katika miezi hii.
Jaribu kumridhisha Allah (عَزَّوَجَلَّ) na usipate ghadhabu yake kwa kumuasi.
Yote niliyoyaeleza hapo juu ni tisa, kumi yake si nyingine bali ni Kufanya Toba, Toba ya kweli kwa Allah. Miezi mitakatifu imeanza hivyo ni wakati wa kuomba msamaha kwa dhambi zote tulizotenda. Haya ni pamoja na shirki, kutowatii wazazi, kuvunja undugu, kula riba, uwongo, kuzungumza nyuma ya mgongo wa mwingine (kusengenya), wivu, n.k
Nikimalizia, nimalizie kwa maneno yenye manufaa ya Ibn Rajab ( Rahimahullah)
“Iwapo mtu hawezi kutenda mema katika miezi hii basi angalau ajiepushe na maovu na aihurumie nafsi yake. Hii ni pamoja na kutokufanya udhalimu.” Mfano wa uonevu huo ni kuwadhulumu wazazi na watoto, wanandoa kudhulumiana, kula mali ya yatima, kuiba, kuhonga n.k..”
Naamini mpaka hapa ushafahamu namna unaeza idhulumu nafsi yako. Na naamini hautajidhulumu tena siku za usoni.
Nafurahi nikuone tena akhy yangu katika makala ijayo, na tafadhali usikose. Kama bado hujasubscribe, itapendeza ukifanya sasa, kwani In shaa Allah mazuri yanakuja.
Pia ningependa unipe maoni yako juu ya makala hii, umefaidika?, Au unalipi la kuniambia akhy/ukhty yangu. Usijali, kuwa huru njoo tupige story kupitia WhatsApp yangu, Bofya Hapa!
Jazakallahu khayr, Assalam alaykuuum..!
Ni Mimi Akhy yako Mubaarak kutoka Ahadun Ahad Studio, Onja Ladha Ya Imaaan!