Ukizingatia Matatu(3) Haya, Hautakuwa Na Hofu Wala Huzuni Maishani Mwako..
Niliishi kwa wasiwasi, hofu na huzuni nikihofia nisikutwe na mabaya, lakini nilipozingatia matatu (3) haya, hofu iliniisha. Shuka nami nikueleze nawe SIRI hizi!
Bismillah Rahman Raheem
Assalam alaykum msomaji wangu mpendwa, karibu tena katika makala hii yako pendwa inayoandikwa na Mimi Akh. Mubaarak..
Kama ndio mara ya kwanza hapa, basi nikuombe usubscribe ili usikose Faida nyingi zijazo..
Naam..
Kutokana na maisha jinsi yalivo hakuna anaependa kuishi kwa hofu na Huzuni..
Naamin hata wewe hupendi hivo..
Na ajabu ni kuwa Hata Yule aliekuumba wewe na Mimi hapendi kuona upo katika hofu au huzuni
Na kutokana na hilo akatueleza Allah namna ya kuepukana na hofu..
Ili ukiishi kwa hofu iwe umejitakia mwenyew kwa kutokuijua SIRI hii, au kuipuuza..
Allah subhana anasema..
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ } بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
[Surah Al-Baqarah: 62]
Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.(Duniani na Akhera)
Kama nilivosema mwanzo, kuwa maisha yetu ya Leo kumejaa mambo yenye kuleta huzuni, wasiwasi, mashaka na hofu..
Ambayo hofu hii na huzuni kwa namna moja au nyingine hupelekea mtu kupata maradhi mbalimbali ikiwemo Msongo wa mawazo, sonona n.k..
Kwa hivo, ili kujiokoa na madhara ya huzuni na wasiwasi hizo..
Yapasa tufuate kile ambacho Allah ametuelekeza katika Qur'an yake, katika Aya nilioitaja hapo nyuma..
Aya imetaja mambo 3 ya kuzingatia..
Nayo ni..
1. Kumuamini Allah
2. Kuamini siku ya hukum(ya mwisho)
3. Kutenda mema
Ukifikiria points hizi 3 kwa kina, utagundua kuwa points 2 za mwisho zinategemea katika point namba moja..
Kivipi?, Ngoja tuone..
Kama matendo yetu si ya sawa, na Imani zetu juu ya siku ya mwisho ni dhaifu, basi ni dhahiri kuwa hata Allah hatujamuamin kiukweli..
Na ikiwa tunafanya matendo mema, na Imani zetu juu ya siku ya mwisho zikaimarika. Basi hata Imani yetu kwa Allah itakuwa thabiti zaidi..
Na Kumuamini Allah Kwa namna gani kutatutoa katika hofu na Huzuni?..
Huku ni uamini kuwa..
قُلْ لَنْ يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا ۚ وَعَلَى اللَّهِ { فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ
[Surah At-Tawbah: 51]
Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia Allah. Yeye ndiye Mungu wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Allah tu!
Naam, yaani ni kwamba
"Lililokupata (baya/zuri) ni Allah amekuandikia, na lililokukosa (baya/zuri) ni Allah amekuandikia.."
Pia Rasulullah Salallahu alayh wa salam anatuambia..
"Hautaonja Ladha ya Imaani mpaka ujue lile lililokupata halikuwa likukose, na lile lililokukosa halikuwa likupate.."
Ukiwa na imaani hio utasahau kama kuna kitu kinaitwa "hofu" au "wasiwasi"!
Na ndo maana utakuona Rasulullah Salallahu alayh wa salam wakat anahama kwenda Madina..
Licha ya kuwa Makuraysh walikuwa wakimfuata ili wamzuie kwenda Madina na wamuue..
Hakuwa na hofu wala wasiwasi, alifika katika pango yeye na Abu Bakar na akapatwa na usingiz..
Abu Bakar Radhiyallahu anhu anamwambia Rasulullah Salallahu alayh wa salam..
"Yaa Rasulullah, hapa pangoni hawa Makuraysh wakija watatuona.."
Rasulullah akamjibu Abu Bakar, "Ewe Abu Bakar, waonaje wawili, watatu wao akawa ni Allah?"
Akimaanisha usiwe na hofu, muamini Allah..
Pia Kumuamini Allah Kwa yale aliotuamrisha na kuacha Yale aliotukataza..
Na tufuate vile alivotuelekeza Rasulullah Salallahu alayh wa salam..
Katika kufuata hayo tunaepukana na hofu, wasiwasi na majuto ya hapa Duniani na Akhera..
Pia Kumuamini Allah Kwa yale aliotuamrisha na kuacha Yale aliotukataza..
Na tufuate vile alivotuelekeza Rasulullah Salallahu alayh wa salam..
Katika kufuata hayo tunaepukana na hofu, wasiwasi na majuto ya hapa Duniani na Akhera..
Pia, tusisahau points 2 za mwisho..
Katika kuamini siku ya mwisho, hii inamaana ujiandae na siku hii..
Na katika kujiandaa na siku hii ni kufanya yale ambayo yatakuepusha na Huzuni na majuto ya siku hii..
Lipa haki za Allah na za watu Kabla hujaenda lipishwa siku hio..
Ukiishi kwa kuamini kuna siku ya hukum..
Utaishi kwa uadilifu na kuchunga haki za watu..
Ukiwa hivo, ni ngumu kuwa na hofu na wasiwasi kwakuwa hakuna anaekudai..
Tatu, matendo mema..
Kujitendea wema nafsi yako Kwa kutoidhulumu kwa kuifanyia maasia..
Kuwatendea wema watu Kwa kuwajali, kuwaheshimu, kuwapenda, kuwasaidia kadri ya uwezo n.k..
Hofu itakuondoka..
Kwa maana ukiishi hivo..
Utakuwa huna baya, mtu wa watu..
Amani kabisa Maa Shaa Allah..
Uwe kama Yusuf alayh salaam..
Ameishi na watu vizuri mpaka wakafikia kusema.. "Yusuf hana baya.."
{ قُلْنَ حَاشَ لِلَّهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ مِنْ سُوءٍ }
[Surah Yûsuf: 51]
Wakasema: Hasha Lillahi! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake..
Naam, hadi hapo ndugu yangu, sina la kuongeza.
Tukishikamana na hayo hata depression zitapungua, Biidhnillah..
Ni mimi Mubaarak..
Assalam alaykum!
Allah akuhifadhi msomaji wangu mpendwa!