Hakika Mi Naisikia Harufu Ya Yusuf...
Usikate Tamaa Juu ya Hustle zako, Usihuzunike juu Ya unayopitia, Amini katika harufu ya Yusuf na mtegemee Allah. Ni Ipi harufu ya Yusuf??, Shuka nami..
Surat Yusuf, Ni Surah ambayo inamafunzo mengi mno hakika, hasa kwetu vijana. Nilishawahi kuizungumzia hapo kabla. nitaweka link mwisho uipitie nayo..
Lakini..
Miongoni mwa mafunzo ninayojifunza kupitia Surat Yusuf, ambayo nakuandikia ili nawe ndugu yangu uijue..
Ni kuamini kuwa lile unaloamini linawezekana, basi litawezekana Biidhnillah! Na kuto kukata kataa..
Hata kama kwa macho ya kawaida na fikra za kawaida linaonekana haliwezekani, Ila we amini linawezekana Biidhnillah!
Hata kama utakosa support, Lakin kwa uwezo wa Allah amini linawezekana..
Huenda unayo mipango, fikra, mitazamo flan ambayo si mibaya, si ya haraam, pengine ya biashara au ya kimaisha..
Lakin ukiwaeleza watu wako wa karibu, au watu unaowaamin wanakukatisha tamaa, au pengine wanakuona umekosa vya kufikiria..
Ni kuamini kuwa lile unaloamini linawezekana, basi litawezekana Biidhnillah! Na kuto kukata kataa..
Lakin, ukimuangalia Mzee Yaaqub ndani Surat Yusuf, we fikiria, Mzee amepotezewa mwanae anaemkubali kuliko wanae wote..
Na hajui hata alipo, hajui amekufa au yupo hai, hajui kama ni mtumwa au yupo huru. Ila ye aliamin ATARUDI..
Na kila alipokuwa akimuongelea Yusuf mbele za Kaka zake, walimuona “huyu Mzee anazeeka vibaya wallah..”😒
Miongoni mwa aya ninayoipenda ni pale Mzee Yaaqub aliposema..
{ إِنِّی لَأَجِدُ رِیحَ یُوسُفَۖ لَوۡلَاۤ أَن تُفَنِّدُونِ }
[Surah Yūsuf: 94]
“Mimi nasikia harufu ya Yusuf, lau kama hamtaniona mi mwendawazimu..”
Katika Aya hii, Mzee Yaaqub anawambia wanae, wajukuu zake pengine.. Mi nasikia harufu ya Yusuf, mi naamin Yusuf atarudi, mi naamin nitamuona tena Yusuf, hata kama nyie mtaniona mi mwendawazimu, nazeeka vibaya..
Wanae sasa, wala hata hawakumpa hope, wala hawakujali katika maono yake, ndo kwaanza wakamwambia..
{ قَالُوا۟ تَٱللَّهِ إِنَّكَ لَفِی ضَلَـٰلِكَ ٱلۡقَدِیمِ }
[Surah Yūsuf: 95]
Wakasema, wallah, we mzee bado upo katika ule upotevu wako, wendawazimu wako wa kudhani Yusuf atarudi..
Na hio ndo Hali Halisi ya maisha, Ila wewe amini katika harufu ya Yusuf, harufu ya mafanikio yako katika jambo unaloamini litakuwa, huenda harufu hio utaisikia peke yako..
Ukiwaeleza wengine watakuambia kama wanae walivomuambia Mzee wao Yaaqub, ukawa heart breaked bure..💔
Kuna Hadeeth Rasulullah Salallahu alayh wa salam anasema
“Mfunge ngamia wako, kisha muamini Allah..”
Hivo katika mipango yako, mitikasi yako, harakat zako, “Mfunge ngamia”, Yan fanya asbaab, alaf muachie Allah amalize kazi..
Mzee Yaaqub aliamin Yusuf atarudi, alimiamini atamuona tena, na hivo hakukata tamaa, ndo akawaambia wanae..
{ يَٰبَنِيَّ ٱذۡهَبُواْ فَتَحَسَّسُواْ مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَاْيۡـَٔسُواْ مِن رَّوۡحِ ٱللَّهِۖ }
[Surah Yūsuf: 87]
Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraji ya Allah..
Yani, hakuacha kufanya asbaab ya kupatikana kwa Yusuf, na aliamin kwa uwezo wa Allah atampata, na kweli akampata Biidhnillah, Alhamdulillah..
Kwahivo tusikate tamaa katika kile tunachokiamin katika mafanikio, hata kama dalili hazionekani, Lakin kwa uwezo wa Allah kila kitu kitakaa sawa..
Nadhani umenielewa mpendwa, Allah akubaarik..
Assalam alaykum!🥂
Unaweza ukasoma article niliowahi kuandika kuhusu Surat Yusuf na mafunzo yake click hapa