Jinsi Ya Kwenda Hija, Bila Kutumia Hata Senti..!🤫
Unatamani kwenda Hija, lakini pesa ndo kipengele?, Si ndio? , Usijali, Shuka nami nikupe njia za kwenda Hija bila kupoteza hata senti.. (100% Proved)
Assalam alaykum, Vipi hali yako akhy/ukhty yangu..
Mpaka umefungua makala hii, inaashiria kwamba unatamani kujua namna unaweza Hiji bila kutumia pesa, si ndio Akhy/Ukhty?
Kama jibu ni ndio, basi wala usijali Akhy yangu. Ndani ya dakika chache zisizozidi 4 zijazo, nitakufahamisha namna unaweza fanya hivo, cha msingi ni uwe nami mpaka Mwisho wa makala hii. Na naamin utafaidika.. Tusema Inshaa Allah..
Sawa, Lakini Akhy/Ukhty yangu kabla sijaanza kukuonesha njia, nikuombe usubscribe katika makala hii, ili usikose Faida kama hizi siku zijazo, kupitia email yako, subscribe kisha tuendelee.
Tayari ee?, Haya, hongera MaaShaa Allah kama tayari, Allah akubaarik!
Basi wala nisikuchoshe Akhy/Ukhty, njia zenyewe ni simple Tu, ni njia ambazo ametufundisha Mtume Muhammad Salallahu alayhi wa salam.
Nazo ni..
Kusema Tasbih, Tahmid na Takbir kila baada ya swala ya Faradh.
Naam, hio ni moja ya njia unazoweza tumia ukapata ujira sawa na yule aleenda Hajj, kwa wewe kukaa katika mswala wako ukimtaja Allah, unakuwa sawa na mwenyekuhiji, Allahu Akbar!, na kuthibitisha hilo, anasema Rasulullah salallahu alayhi wa salam katika Hadith..
Abu Huraira (r.a) amesema: “Baadhi ya watu masikini walikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakasema: “Watu matajiri watapata daraja za juu na watapata starehe ya kudumu kwakuwa wanaswali kama sisi na kufunga kama sisi. Wana pesa nyingi zaidi wanazotumia kwenda Hija na Umra, na kupigana (katika Njia ya Allah) na kutoa sadaka."
Mtume (Salallahu alayhi wa salaam) akasema: “Je, nisikuambieni jambo ambalo mkilitenda mtawapata walio kupita kwenu? Hakuna mtu ambaye atakupateni na atakuwa bora kuliko watu unaoishi kati yao, isipokuwa wale ambao wangefanya vivyo hivyo. (Ukisema) SubhanAllah, Alhamdulillah na Allahu Akbar mara thelathini na tatu kila baada ya kila swala (ya faradhi)“’.1
Kuchukua Wudhu, kisha kwenda kuswali Swala Ya Faradh Msikitini
Ukifanya hivi katika mwezi huu wa Dhul Hijja utakuwa unapata ujira sawa na aliekwea pipa hadi Makkah, Ujira sawa kabisa. Na kama utaendelea kufanya hivi katika Miezi mingine utapata ujira sawa na alienda Umrah. Allahu Akbar!, Unaona mambo yalivokuwa mepesi, ni Nia yako, na kujituma kwako katika Ibada kwa ajili ya Allah..
Kuthibitisha hili amesema Rasulullah salallahu alayhi wa salam
“Mwenye kutoka nyumbani kwake baada ya kutawadha na akaenda kuswali Swalah ya faradhi Msikitini, malipo yake yatakuwa kama ya mwenye kwenda kuhiji baada ya kuvaa Ihraam. Na anayetoka kwenda kuswali Swalah ya Dhuha, na akajishughulisha kwa ajili Nia hiyo pekee, basi atapata malipo kama ya mtu anayefanya Umra..”2
Kuswali Swala ya Ishraq
Swala ya Ishraq, ni swala inayoswaliwa baada tu ya Jua kuchomoza. Hivo ukiamka asubuhi, ukaswali Fajr kwa jamaa, ukafanya Dhikr mpaka jua likachomoza kisha ukaamka ukaswali rakaa 2 za Ishraq na wewe utakuwa ni sawa na Umeenda Hija na Umrah, kwasababu ya Ujira utakao upata. Umeona Akhy/ukhty, Umetumia pesa ngapi hapo?, Hahaha..
Anasema Rasulullah salallahu alayhi wa salam..
“Mwenye kuswali Alfajiri kwa jamaa, kisha akakaa kwa kumdhukuru Allah mpaka jua lichomoze, kisha akaswali rakaa mbili (Swala ya ́Ishraq), basi kwake yeye ana malipo kama ya Hajj na Umrah'. [Tirmidhi]3
Kwenda Msikitin kujifunza dini au kuifundisha..
Naam akhy/ukhty, miongoni mwa njia ambazo unaweza Tumia kwenda Hija na Umrah ni hio ndugu, kujilazimisha na kushikamana na darsa za wanawazuoni, Kutoka kwako Nyumbani kwako hadi msikitini ili kujifunza dini yako unapata ujira sawa na alietoka nyumbani kwake hadi Makka!, Allahu Akbar, hata hili likushinde ndugu yangu?, Allah akuongoze..
Anasema Rasulullah salallahu alayhi wa salam..
Yeyote anayekwenda msikitini kwa madhumuni ya kujifunza au kufundisha mema, anapata ujira wa mwenye kuhiji aliyemaliza Hijja yake..4
Hitimisho..
Naam Akhy, Mimi naishia hapo Akhy, naamini nimekukumbusha jambo katika hilo. Na hivo usiwe mnyonge kwa kuwa huna kipato cha kufanya Hija na Umrah. Kama Allah amekujaalia unaeza swali na Una afya hio ni Baraka tosha..
Tafuta njia miongoni mwa hizo njia nyepesi hapo juu, zisizokugharimu hata Shs1/= na Ishi nazo, na kwakufanya hivo huenda wewe ukamzidi Ujira Yule aleenda Makka, huez jua bana Allah ndie mgawaji wa Fadhla na Thawabu..
Ila Kabla Hujaondoka..
Kabla Hujaondoka niskize kidogo..
Kwanza, usisahau kujizatiti na kupupia katika Ibada katika makumi haya ya Dhul-Hijja, Ikiwemo kufanya Ibada kama hizo nilizozieleza hapo mwanzo. Allah akuongoze katika hilo..
Pia, Kama hukusubscribe Akhy, Nikukumbushe na kukusisitiza ufanye hivo. Ili upate Faida na ukumbusho kama huu kupitia email yako.
La mwisho nikuwa, naamin umepata Faida, na naamini kutokana na ukumbusho huu unacho cha kuniambia, basi wala usisite kuniambia unachowaza, au maoni. Niambie kupitia WhatsApp yangu, hapa..
Ni Mimi Akhy yako Mubaarak, Kutoka Ahadun Ahad Studio, Onja Ladha Ya Imaan
Riyad as-Salihin 1418, Rejea ndani ya Kitabu; Kitabu #15, Hadith 11.
Sunan Abi Dawud 558, Kitabu #2, Hadith 168.
Imepokewa na At-Tirmidhiy na imepewa daraja Hasan na al-Albani katika Swahiyh Tirmidhiy nambari. 586]
Mukhtasari wa Al-Hadith Al-Albani, hukumu ya Hadith ni Hasan Sahih katika Sahih Al-Targheeb 86.
Pia angalia : al-Mu’jam al-Kabīr 7346